SEM-BT ni kikundi cha watu wachache ambacho kinatoa huduma zake hapa tanzania
Kikundi cha SEM BAND – TANZANIA (SEM-BT) ambacho kimesajiliwa kisheria kwa
namba za usajili CDC/CSO/114/2019, ambacho
makao makuu yake ni Chato kati karibu na ilipokuwa ofisi ya TANESCO, kinajishughulisha
na shughuli za kuandaa matamasha
mbalimbali ya uimbaji wa nyimbo ikiwa ni
pamoja na kuziweka katika mfumo wa sauti na Video na kuuza DVD ili kujipatia
kipato. Pamoja na kuwaunganisha vijana kuwa pamoja katika shughuli mbalimbali
za kiuchumi, kidini na kijamii.
Kikundi hiki kilianzishwa tangu mwaka 2016 ambapo kilikuwa na watu wawili tu na kazi zake ilikuwa ni kuwaunganisha watu mbalimbali katika matamasha mbalimbali ya kidini na kijamii. kikundi hki hakikuweza kuendelea zaidi kutokana na kukosa pesa za kuendeshea kikundi. Mwaka 2019 waasisi wa kikundi hiki waliamua kushirikisha wadau wengine ili kuweza kurekodi na tulifanikiwa kurekodi nyimbo mbili kwa mfumo wa sauti na video pia (Nyimbo hizo ni ("Basi iweni na huruma" uliotungwa na E.Ogeda pamoja na "Tuwe na moyo wa majitoleo" uliotungwa na E.Nyanza). Mpaka sasa hivi tunajiandaa kuzisambaza hizo nyimbo zetu kwa njia ya you tube na mitandao mingine ya kijamii muda si mrefu. kaa tayari kuzipokea.
Endelea kutufuatilia kwani tutakuletea mambo mengi mazuri kwa siku zinazokuja.
Emmanuel. Shimbala
Katibu SEM-BT
No comments:
Post a Comment