Wednesday, February 12, 2020

FAIDA ZA KUIMBA KWA AFYA YAKO



Habari za leo ndugu msomaji wa SEM-BT?


Leo nitaongelea kuhusu faida za kuimba ambazo zinamsaidia mtu kiafya.

Kwanza kabisa naomba nikueleze maana ya kuimba.

KUIMBA ni kutoa sauti yenye ulinganifu, sauti hiyo inatakiwa kufuata mapigo ya ki muziki na ni zaidi ya kughani. Zamani mababu zetu walikuwa wanaimba kwenye kazi mbalimbali ili kurahisisha kazi yenyewe iliyokuwa ikifanyika, mpaka sasa watu wengi huimba ili kuburudisha, kufundisha, kukosoa au kuelimisha kikundi fulani cha watu.

Kuimba ni faida kwa mwimbaji kwani kuna faida nyingi saana ambazo mwimbaji anazipata kama vile kuburudika, kuburudisha, kuinjilisha, kuhamasisha, kufariji, kufurahisha n.k

Leo nitakueleza faida za kuimba ambazo zinamsaidia mwimbaji kiafya, Faida zenyewe ni:

  1. Kuimba ni mazoezi. Unapoimba unafanya mazoezi ambayo pia ni kinga kwa magonjwa mbalimbali yanayoweza kumuathiri mtu ambaye hafanyi mazoezi. Mazoezi ambayo nayasemea hapa ni Kupanua kiwambo (diaphragm), mwanakwaya anatumia nguvu nyingi sana wakati anaimba ili kupanua mapafu na kiwambo. Hii itamsaidia mwimbaji ku zuia magonjwa yanayoweza kuathiri mapafu kama vile kikohozi, mafua.
  2. Inasaidia kuboresha mfumo wa upumuaji mwilini kwani msukumo wa damu utakuwa mkubwa ambapo ndani ya chembe za damu huwa kuna hewa safi ya Oxygen ambayo husambazwa mwilini pote na chembe za damu katika mzunguko. 
  3. Inasaidia kupunguza mawazo. Hili liko wazi kabisa  kwa mwanakwaya au mwimbaji yeyote yule, ukiimba unapunguza mawazo. Mtu mwenye mawazo anaweza kuugua hata magonjwa ya akili na kisaikolojia.
  4. Husaidia kusimama vizuri. Mwimbaji huwa ana staili yake ya kusimama ambapo kifua chake anakiweka mbele, mabega yanakuwa yameinuka kidogo ili kumsaidia kutoa sauti, mgongo pia unakuwa umenyooka vizuri. Hii inamsaidia kuufanya uti wa mgongo usijikunje. Kwa hiyo mwanakwaya anapoimba kwa muda mrefu huwa na tabia ya kusimama kama anataka kuimba na hivyo kumsaidia yeye kutunza na kukinga uti wa mgongo.
  5. Huimarisha mfumo wa kinga mwilini. (strengthen the immunity system) Kwenye      mwili wa binadamu kuna kinga (protini) ambayo ina jina la kitaalamu ambalo ni Immunoglobulins, kwa hiyo mtu anapoimba anafanya mazoezi (kama nilivyosema hapo juu) na unapofanya mazoezi ina maana kwamba unaongeza kinga mwilini tofauti na mtu ambaye amekaa tu bila kufanya mazoezi



Kwa ufupi sasa kuimba kuna faida kiafya, faida zingine nimezitaja hapa chini ambazo ni:

  • Kuimba nidawa ya asili ya mawazo (natural annti-depresant)
  • Kuimba kunapunguza mawazo kwa kiasi kikubwa sana (ni dawa kwa mtu mwenye mawazo)
  • Kuimba kunaongeza uwezo wa kufikiri na kuchukua maamuzi.

Faida za kuimba kwenye jamii.


  1. Kuimba humsaidia mtu kuongeza idadi ya marafiki.
  2. Kuimba kunamwongezea mtu kujiamini katika kila kitu anachokifanya kwa faida yake na jamii kwa ujumla.
  3. Kuimba kunapanua wigo wa mawasiliano.
  4. Kuimba humsaidia mtu kuwa na hisia juu ya kile anachokiimba.
  5. Kwa wanakwaya wa nyimbo za dini, kuimba kunamweka karibu na Muumba wake.
Kwa leo naomba niishie hapo, nakutakia kila la heri katika majukumu mbalimbali ya kujenga taifa na jamii yetu kwa ujumla. Nakuomba pia uendelee kuka mkao wa kusubiria kazi ambayo tutaitoa hewani muda si mrefu, ni nyimbo mbili ambazo tulizirecord kwa mfumo wa sauti na video.


Imeandikwa na;
SEM BAND TANZANIA
CHATO-GEITA TANZANIA
+255 762 176 662 au +255 756 446 979
E-mail: sembandtanzania@gmail.com 


No comments:

VITU KUMI HATARI KWA AJILI YA SAUTI YAKO.

Nakushukuru ndugu msomaji wangu kwa kuendelea kufuatilia makala hizi.  Nilikuwa naongea na  Tabibu kutoka Hospitali ya wilaya ya C...